Ufunuo wa Yohana 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ufunuo wa Yohana 8 (Swahili) Revelation 8 (English)

Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa. Ufunuo wa Yohana 8:1

When he opened the seventh seal, there was silence in heaven for about half an hour.

Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba. Ufunuo wa Yohana 8:2

I saw the seven angels who stand before God, and seven trumpets were given to them.

Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi. Ufunuo wa Yohana 8:3

Another angel came and stood over the altar, having a golden censer. Much incense was given to him, that he should add it to the prayers of all the saints on the golden altar which was before the throne.

Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika. Ufunuo wa Yohana 8:4

The smoke of the incense, with the prayers of the saints, went up before God out of the angel's hand.

Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi. Ufunuo wa Yohana 8:5

The angel took the censer, and he filled it with the fire of the altar, and threw it on the earth. There followed thunders, sounds, lightnings, and an earthquake.

Na wale malaika saba wenye baragumu saba wakajifanya tayari ili wazipige. Ufunuo wa Yohana 8:6

The seven angels who had the seven trumpets prepared themselves to sound.

Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea. Ufunuo wa Yohana 8:7

The first sounded, and there followed hail and fire, mixed with blood, and they were thrown to the earth. One third of the earth was burnt up,{TR omits "One third of the earth was burnt up"} and one third of the trees were burnt up, and all green grass was burnt up.

Malaika wa pili akapiga baragumu, na kitu, mfano wa mlima mkubwa uwakao moto, kikatupwa katika bahari; theluthi ya bahari ikawa damu. Ufunuo wa Yohana 8:8

The second angel sounded, and something like a great burning mountain was thrown into the sea. One third of the sea became blood,

Wakafa theluthi ya viumbe vilivyomo baharini, vyenye uhai; theluthi ya merikebu zikaharibiwa. Ufunuo wa Yohana 8:9

and one third of the living creatures which were in the sea died. One third of the ships were destroyed.

Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka juu ya theluthi ya mito, na juu ya chemchemi za maji. Ufunuo wa Yohana 8:10

The third angel sounded, and a great star fell from the sky, burning like a torch, and it fell on one third of the rivers, and on the springs of the waters.

Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu. Ufunuo wa Yohana 8:11

The name of the star is called "Wormwood." One third of the waters became wormwood. Many people died from the waters, because they were made bitter.

Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya jua ikapigwa, na theluthi ya mwezi, na theluthi ya nyota, ili kwamba ile theluthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake, wala usiku vivyo hivyo. Ufunuo wa Yohana 8:12

The fourth angel sounded, and one third of the sun was struck, and one third of the moon, and one third of the stars; so that one third of them would be darkened, and the day wouldn't shine for one third of it, and the night in the same way.

Kisha nikaona, nikasikia tai mmoja akiruka katikati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya nchi! Kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu za malaika watatu, walio tayari kupiga. Ufunuo wa Yohana 8:13

I saw, and I heard an eagle,{TR reads "angel" instead of "eagle"} flying in mid heaven, saying with a loud voice, "Woe! Woe! Woe for those who dwell on the earth, because of the other voices of the trumpets of the three angels, who are yet to sound!"